Home Sports RATIBA YA SIMBA FEBRUARI NI NGUMU KWELIKWELI

RATIBA YA SIMBA FEBRUARI NI NGUMU KWELIKWELI

WACHEZAJI wa Simba wanaratiba ngumu kwelikweli ndani ya mwezi huu mpya wa Februari katika kusaka matokeo kutokana na ratiba kwao kuwa mwendo wa bandika bandua.

Mabingwa hao watetezi wakiwa nafasi ya pili na pointi zao 25 kesho Februari 03 wanakazi ya kuanza kusaka ushindi mbele ya Wajelajela, Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa.

Simba inakumbuka kwamba msimu wa 2020/21 walipokutana Uwanja wa Mkapa dhidi ya Prisons walipata tabu kupata pointi moja katika sare ya kufungana bao 1-1 kwa kuwa bao la Simba lilifungwa dakika za lala salama.

Mbali na ugumu wa kupenya mbele ya Prisons rekodi zinaonyesha kwamba timu hiyo ipo nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi na pointi zake ni 11 hivyo inapambana kujinusuru kwenye nafasi ya mstari mwekundu.

Februari 6 itakuwa ni dhidi ya Mbeya Kwanza iliyo nafasi ya 12 na pointi zake 12 baada ya kumaliza kete zake mbili za kwenye ligi inakwenda kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho ambapo itaanza dhidi ya Asec Mimosas itakuwa Februari 13.

Ikiwa na presha kubwa ya kutusua kimataifa katika hatua ya robo fainali itakutana na USGN Februari 20 kisha kigongo cha mwisho itakuwa ni RS Berkane Februari 27 hapa watakutana na Tuisila Kisinda mzee wa spidi 120 ambaye aliwahi kucheza ndani ya Yanga.

Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco aliliambia Championi Jumatano kuwa ratiba yao ni ngumu lakini hawana namna watapambana.

“Ukitazama ratiba kwetu ni ngumu kutokana na mechi zake ambazo tutacheza na tumetoka kucheza mechi tatu ugenini ambazo hatukupata matokeo mazuri, kikubwa ambacho tunakifanya kwa sasa ni kutafuta matokeo kwenye mechi zetu zijazo,”.

Previous articleMASON MAJANGA MATUPU, UNITED WAMUONDOA
Next articleHII HAPA RATIBA YA MZUNGUKO WA 14,SIMBA MIKONONI MWA WAJELAJELA