Home Sports DAKIKA 45,KIRUMBA,YANGA 0-0 MBAO FC

DAKIKA 45,KIRUMBA,YANGA 0-0 MBAO FC

UWANJA wa CCM Kirumba, milango bado ni migumu kwa timu zote mbili katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora.

Ni Yanga ambayo ulitinga hatua ya fainali na Mbao FC ya Mwanza ambayo inashiriki First League.

Kipa Aboutwalib Mshery dakika ya 44 aliweza kufuta makosa yake kutokana kurudishiwa mpira na mchezaji wa Yanga.

Hakuna timu ambayo imepiga shuti lililolenga lango nà ni shuti mojamoja kwa timu hizo lilikwenda nje ya 18.

Kona Yanga wamepiga 8 huku Mbao FC ikiwa haijapiga kona ndani ya dakika 45 za kipindi cha mwanzo.

Previous articleADAMA AREJEA NYUMBANI KWA MARA NYINGINE
Next articleYANGA HAO 16 BORA,MAYELE ATUPIA