Home Sports ADAMA AREJEA NYUMBANI KWA MARA NYINGINE

ADAMA AREJEA NYUMBANI KWA MARA NYINGINE

NYOTA wa Wolves, Adama Traore amejiunga na Barcelona kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu huu kuitumikia timu hiyo.

Nyota huyo alikuwa amewekwa kwenye hesabu na Kocha Mkuu wa Spurs, Antonio Conte hivyo kuibuka kwake ndani ya Barcelona maana yake ni kwamba imekula kwake sasa.

Conte aliweka wazi kwamba anataka kuboresha kikosi chake lakini Spurs inaingia katika dirisha la usajili ikiwa katika siku za mwisho bila kufanya usajili.

Barcelona wameinasa saini ya nyota huyo mwenye mwili jumba na wameweka ofa ya kumnunua moja kwa moja kwa pauni milioni 30 mwishoni mwa msimu ikiwa atawafurahisha.

Nyota huyo aliwahi kuwa ndani ya Barcelona mwaka 2015 akajiunga na Aston Villa kisha Middlesbrough na akatua Wolves 2018.

Previous articleKIKOSI CHA YANGA DHIDI YA MBAO FC
Next articleDAKIKA 45,KIRUMBA,YANGA 0-0 MBAO FC