Home Sports SIMBA QUEENS KAZINI LEO DHIDI YA MLANDIZI QUEENS

SIMBA QUEENS KAZINI LEO DHIDI YA MLANDIZI QUEENS

LEO Januari 28,2022 Simba Queens inakibarua cha kusaka ushindi mbele ya Mlandizi Queens.

Ni mchezo wa Ligi ya Wanawake ambayo inaendelea na unatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni.

Simba Queens ni mabingwa watetezi wanakutana na Mlandizi Queens ambayo itawakosa baadhi ya nyota wao ambao wamejiunga na timu ya taifa U 20.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Bunju Complex.

Kwa upande wa Simba Queens ni pamoja na Opah Clement na Fety Densa na kwa mastaa wa Mlandizi ni pamoja na kipa Niwael Makuruta.

Previous articleHAWA HAPA WAKALI WA KUCHEKA NA NYAVU SIMBA
Next articleSIMBA YAIVUTIA KASI DAR CITY