Home Sports HAWA HAPA WAKALI WA KUCHEKA NA NYAVU SIMBA

HAWA HAPA WAKALI WA KUCHEKA NA NYAVU SIMBA

LICHA ya Klabu ya Simba kuanza vibaya msimu huu wa NBC Premier League, mshambuliaji wa klabu hiyo Meddie Kagere ameendelea kuweka rekodi zake ngumu ndani ya kikosi hicho kwa kufunga magoli mengi msimu huu.

Klabu ya Simba mpaka sasa wamecheza jumla ya michezo 13 ya NBC Premier League , katika michezo hiyo Meddie Kagere amefunga jumla ya mabao manne na ndiye kinara wa magoli msimu huu ndani ya kikosi cha Simba.

Nafasi ya pili ya ufungaji bora ndani ya klabu ya Simba inashikiliwa na mshambuliaji mpya wa timi hiyo Kibu Denis ambaye amejiunga na Klabu ya Simba akitokea katika Klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya.

Kibu Denis yeye amefanikiwa kufunga jumla ya magoli matatu kwenye michezo 13.

Wachezaji wengine kama vile Mzamiru Yassin, Kanoute, Sakho, Mohammed Hussein, Peter Banda na Rally Bwalya wamefunga bao moja moja msimu huu.

Takiwimu hizi siyo siyo mbaya sana kwa msimu huu licha ya kwamba hazina uwiano mzuri na takwimu za msimu uliopita ambapo Simba Sc walikua na uwezo mkubwa wa kufunga magoli mengi wakiwa na washambuliaji wao hatari Chris Mugalu, Meddie Kagere, na Bocco ambao msimu huu wamekua na kiwango kibovu kwa kushindwa kufunga.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA
Next articleSIMBA QUEENS KAZINI LEO DHIDI YA MLANDIZI QUEENS