KOCHA Mkuu wa Chelsea, Thomas Tuchel juzi alikataa kujibu maswali ambayo yalikuwa yanamhusu staa wa timu hiyo Romelu Lukaku akisema sio tatizo ndani ya timu hiyo.
Tuchel ameweka wazi kwamba timu hiyo inapitia wakati mgumu kwa sasa na wachezaji wake wengi wametoka kwenye majeruhi.
Chelsea juzi ilishindwa kutamba kwa mara nyingine na kuambulia sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Brighton ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu England.
Kocha huyo amesema:”Sitaki kujibu maswali juu ya Lukaku. Leo sio kuhusu Lukaku kuna maswali mengi ya kuuliza na sio kuhusu yeye kila wakati.
“Lukaku sio tatizo, ila yeye ndiyo sehemu ya kuwezesha timu kubwa bora.Nimekataa kujibu maswali kuhusu Lukaku kwa sababu naulizwa yaleyale mara 100 zaidi mnatakiwa kuangalia hali halisiya timu,”.