CEDRICK Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga ameweka wazi kwamba kikosi hicho kinazidi kuimarika taratibu kutokana na mechi ambazo wanacheza.
Mpaka sasa ndani ya Ligi Kuu Bara, Yanga haijapoteza mchezo kwenye ligi na inaongoza ligiikiwa na pointi 32.
Jana Januari 18, Yanga ilikuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni FC ambapo iliweza kushinda mabao 2-0 na mtupiaji alikuwa ni Tonombe Mukoko aliyefunga mabao hayo kwa penalti.
Kaze amesema:”Tunazidi kuimarika taratibu na kila mchezaji anajua kwamba kuna jambo ambalo tunahitaji kulifanya na tunazidi kupambana.
“Ushindi mbele ya Mbuni kwetu ni jambo kubwa hasa kuendelea kuwa kwenye hali ya kujiamini zaidi bado kazi inaendelea na tutazidi kupambana ili kupata matokeo zaidi,”.
Miongoni mwa nyota ambao walianza jana ni pamoja na Heritier Makambo huku Chico Ushindi yeye akianzia benhi na aliweza kupata muda wa kucheza pamoja na Crispiin Ngushi ambaye ni ingizo jipya pia kutoka Mbeya Kwanza.