Home Sports KOCHA YANGA AMTAJA MSHERY

KOCHA YANGA AMTAJA MSHERY

KOCHA mpya wa makipa wa Yanga, Mbrazili, Milton Nienov amefunguka kuwa usajili wa kipa, Aboutwalib
Mshery ni usajili bora 
kufanywa na klabu hiyo kutokana na ubora wake,

Kocha huyo ameweka wazi kuwa ameanza na suala la kuhakikisha makipa wa timu hiyo wanahimili presha ya michezo mikubwa.


Milton alitambulishwa 
rasmi na Yanga Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ambapo alikuwa sehemu ya mashuhuda wa mchezo kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga huku Yanga wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Kabla ya kujiunga na Yanga, Milton alikuwa akihudumu kama kocha wa makipa wa Simba kabla ya kuachana nao Oktoba 26, mwaka jana muda mfupi baada ya Simba kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kuhusu kiwango cha makipa wa timu hiyo, Milton amesema:-“Siwezi kuzungumza mengi kuhusiana na uwezo wa makipa wetu kwa sasa, kwa kuwa ndiyo kwanza nimefika hapa lakini katika vipindi vichache vya mazoezi ambavyo nimekuwa pamoja nao naweza kusema tuna makipa bora sana.

“Huyu Mshery ni kijana mdogo na mwenye uwezo mkubwa sana, naamini ulikuwa usajili bora kwetu, niliona alikuwa na presha kidogo kwenye mchezo dhidi ya Coastal na nimepanga kuhakikisha nalifanyia kazi
hilo kwa kuwa ni muhimu 
kwa kipa kuhimili presha ya michezo mikubwa ili kutofanya makosa,”.

Previous articleJEMBE LA KAZI TAYARI KUREJEA SIMBA
Next articleLUKAKU AMFANYA TUCHEL AGOMEE MASWALI