Home Sports SAKHO NA JIMMYSON VIWANGO VYAO VYACHAMBULIWA NA KOCHA WAO

SAKHO NA JIMMYSON VIWANGO VYAO VYACHAMBULIWA NA KOCHA WAO

SELEMAN Matola,Kocha Msaidizi wa Simba ameweka wazi kuwa  viwango vya wachezaji wa timu hiyo ikiwa ni pamoja na  Pape Sakho na Jimmyson Mwanuke vinazidi kuimarika kwa kuwa walifanya vizuri walipopewa nafasi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya JKT Tanzania.

 

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Desemba 14, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Kibu Dennis.

Matola ameweka wazi kuwa Sakho hakuwa uwanjani kwa muda mrefu baada ya kuumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji huku Jimy yeye akikosa nafasi kwenye mechi ambazo zimepita.

“Tumewana namna wachezaji wetu ambavyo wameweza kuonyesha uwezo wao kwenye mchezo ambao walipewa nafasi dhidi ya JKT Tanzania na walifanya kazi nzuri.

“Wamekuwa kwenye viwango bora wanapopata nafasi na tunaamini kwamba wataendelea kufanya hivyo kwa kuwa ushindani ni mkubwa na kila mchezaji lazima apewe nafasi.

“Sakho yeye aliumia kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji hivyo ameanza kuimarika taratibu na Jim yeye hakupata nafasi katika mechi ambazo tumecheza hivyo bado wanazidi kuimarika.

“Maandalizi yetu kwa sasa ni kwenye mechi za ligi kwa kuwa lengo la kusonga mbele kwenye hatua ya mtoano limetimia bado kazi inakuja kwani mcheo wetu ujao utakuwa dhidi ya Kagera Sugar,” amesema.

Mchezo wa Simba dhidi ya Kagera Sugar unatarajiwa kuchezwa Desemba 18, Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi zake ni 18 imetupia mabao nane na moja ni mali ya Peter Banda.

Previous articleIHEFU WATAJA WALIPOELEKEZA NGUVU ZAO
Next articleMSHINDI WA SPORTPESA KUTOKA MOROGORO ASHINDA MKWANJA MREFU