Home Sports IHEFU WATAJA WALIPOELEKEZA NGUVU ZAO

IHEFU WATAJA WALIPOELEKEZA NGUVU ZAO

ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu FC amesema kuwa alikuwa anawalinda wachezaji wake ili wasiweze kuumia kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Mkapa. jana Desemba 15.
Katika mchezo huo Ihefu ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Yanga nawatupiaji walikuwa ni Heritier Makambo ambaye alifunga mabao matatu na Khalid Aucho huyu alitupia bao moja.
Katwila amesema kuwa alibadili kikosi kwa kuwa kuna mchezo mbele wa Championship ambao ni muhimu kwao wakiwa nafasi ya pili.
Katwila amesema:”Kwenye mchezo wa mtoano ukiwekeza nguvu kubwa inaweza kusababisha majeruhi kwa kuwa wachezaji wakipata nafasi ya kuanza lazima wonyeshe uwezo wote.
“Nisingeweza kutolea macho kwenye mchezo wetu kwa kuwa tunashiriki Championship na huku ushindani wake ni mkubwa na malengo yetu ni kuona kwamba tunarudi tena kwenye Ligi Kuu Bara.
“Unaona kwamba baada ya mchezo wetu wachezaji walianza na mazoezi kwa kuwa tunatarajia kusafri na kucheza mchezo wetu dhidi ya African Sports, makosa ambayo tumeyafanya tutafanyia kazi kwa ajili ya mechi zetu zijazo,” .
Kwenye msimamo wa Championship Ihefu FC ipo nafasi ya pili ikiwa imekusanya pointi 23 baada ya kucheza mechi 11, kinara ni DTB wenye pointi 27.
Inakwenda kukutana na African Sports iliyo nafasi ya nane na pointi zake kibindoni ni 15.
Previous articleMTIBWA SUGAR HAWAPOI,WAPIGA MTU KIFURUSHI CHA WIKI
Next articleSAKHO NA JIMMYSON VIWANGO VYAO VYACHAMBULIWA NA KOCHA WAO