Home Uncategorized KIUNGO HUYU KUSEPA MANCHESTER UNITED

KIUNGO HUYU KUSEPA MANCHESTER UNITED

KIUNGO wa Klabu ya Manchester United inayoshiriki Ligi Kuu England, Paul Pogba ataondoka bure ndani ya kikosi hicho msimu wa 2021/22 utakapomeguka kwa kuwa mabosi wa timu hiyo wamethibitisha kwamba hawatamuongezea dili jingine.
Mwishoni mwa msimu huu Pogba mkataba wake utameguka na kuanzia Januari 2022 atakuwa huru kufanya mazungumzo na klabu nyingine ambayo inahitaji saini yake.

United wamesema kuwa kiungo huyo mwenye miaka 28 hatasaini mkataba mpya na timu hiyo wakati ujao na amekuwa akihusishwa kujiunga na Klabu ya Real Madrid na PSG ambazo zinawania saini yake.

Wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola alipoulizwa kama mchezaji huyo atasepa ndani ya kikosi hicho alisema kuwa ni suala la kusubiri na kuona mambo yatakuwaje kwa kuwa kila kitu kipo kimya.

“Ni suala la kusubiri kwa kuwa hadi sasa kila kitu kipo kimya,”

Previous articlePOGBA AFUNGIWA,KOEMAN ATIMULIWA NA REKODI MBAYA
Next articleCITY YAONJA JOTO YA JIWE BAADA YA MIAKA MITANO