Home International CITY YAONJA JOTO YA JIWE BAADA YA MIAKA MITANO

CITY YAONJA JOTO YA JIWE BAADA YA MIAKA MITANO

KLABU ya Manchester City inayonolewa na Kocha Mkuu, Pep Guardiola juzi walitupwa nje kwenye michuano ya Kombe la Carabao kwa mara ya kwanza baada ya kuyeyuka miaka mitano.
City iliweza kuonja joto hilo la jiwe kwa kutolewa kwa mikwaju ya penalti dhidi ya West Ham United baada ya dakika 90 kukamilika kwa timu hizo bila kufungana kwenye Uwanja wa London.

Kiungo Phil Foden aliigharimu City baada ya kuwa mchezaji pekee ambaye alikosa penalti katika mchezo huo uliokuwa ni wa kukata na shoka.Katika mikwaju ya penalti wapinzani wao walishinda penalti zote 5 huku City ikishinda penalti 3 kibindoni.

Mara ya mwisho wa City kutupwa nje katika michuano ya Carabao ilikuwa Oktoba 26,2016 walipoondolewa na Manchester United baada ya hapo walikuwa na zali la kucheza fainali

Previous articleKIUNGO HUYU KUSEPA MANCHESTER UNITED
Next articleKOCHA YANGA AOMBA KAZI SIMBA … SOMA HAPA