AZAM FC YAMALIZWA KIMKAKATI NA YANGA

MABOSI wa Yanga wamebainisha kwamba mkakati wa kuimaliza Azam FC ulishachorwa Songea kwa kuwa walipata muda wa kuitazama timu hiyo ilipocheza mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC.

Azam FC jana ilipoteza mchezo wake wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids FC kwa kufungwa bao 1-0.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha alisema kuwa walipokuwa Songea waliweza kuitazama mechi ya Azam FC dhidi ya Namungo jambo ambalo liawapa nguvu ya kushinda mchezo wao.

“Mkakati wa kushinda mbele ya Azam FC upo  na ulianza tangu tukiwa Songea kwa kuwa tulipata muda wa kuitazama namna Azam FC ilivyoweza kucheza, kiukweli ina timu nzuri na wapo imara ila hilo halitupi tabu.

“Ambacho tunaamini ni kwamba mpango wetu wa kupata pointi tatu unaendelea na kila timu ambayo tutakutana nayo lazima tuonyeshe ushindani kwani tuna jambo ambalo tunataka kukamilisha,”.

Kwenye mchezo wao wa Yanga mabao yalifungwa na Feusal Salum pamoja na Fiston Mayele.