NYOTA wa timu ya taifa ya Tanzania, Simon Msuva ameweka wazi kuwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni ya kila mmoja hivyo anayepewa nafasi ya kuitwa ana nafasi ya kupeperusha vema bendera ya Tanzania.
Msuva hayupo kwenye orodha ya wachezaji waliochaguliwa kuunda kikosi cha Stars kwa ajili ya kuwania kufuzu AFCON 2025 Morocco na katika mchezo uliopita dhidi ya Ethiopita ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Tanzania 0-0 Ethiopia.
Septemba 10 2024 itakuwa kete nyingine ugenini kwa Stars kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Guinea wakiwa ugenini.
Msuva amesema: “Kila mchezaji ana nafasi ya kuwa ndani ya timu ya taifa ya Tanzania kwa sababu ni timu yetu sote, ya Watanzania wote hivyo kila anayeitwa kazi yake ni moja kupambana kwa ajili ya Tanzania.
“Sijaitwa kwenye kikosi cha Stars ipo wazi lakini haina maana kwamba nitakasirika, sitafuatilia wachezaji wakicheza hapana kila mmoja ana nafasi yake na kuitwa inaamanisha kwamba unakwenda kwenye kazi ya Tanzania. Wachezaji walioitwa huwa tunawasiliana nao nina amini watafanya vizuri.”.