>

PATASHIKA HII HAPA BONGO, KITAWAKA

PATASHIKA Bongo haijawahi kupoa kutokana na kila timu kuwa kazini kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja katika dakika 90 za kazi.

Ni Mzizima Dabi mchezo utakaowakutanisha wapinzani wawili Azam FC na vinara wa ligi kwa sasa msimu mpya wa 2024/25 Simba.

Ikumbukwe kwamba Azam FC, Septemba 7 ilimtangaza Rachid Taoussi raia wa Morocco kuwa kocha wake mkuu kwa mkataba wa mwaka mmoja akichukua mikoba ya Yusuph Dabo ambaye alipewa mkono wa asante.

Taoussi amewahi kuvifundisha vilabu mbalimbali Afrika vikiwemo Raja CA, RS Berkane na FAR Rabat vya Morocco, ES Setif na Olympique Khouribga vya Algeria pamoja na timu za taifa za vijana za Morocco.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Azam FC, kocha huyo amekuja na wasaidizi wake watatu, ambao ni kocha msaidizi, Ouajou Driss, kocha wa utimamu wa mwili, Badr Eddine na kocha wa makipa, Rachid El Mekkaoui.

Mchezo wa MzizimaDabi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa itakuwa ni Septemba 26 2024, saa 12:00 jioni.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Dizo Click.