AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa nado hawajafika hata robo ya ubaya ubwela ndani ya kikosi hicho hivyo wapinzani wao wajipange sawasawa.
Ikumbukwe kwamba Septemba 7 2024 Simba ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT Tanzania yenye John Bocco mfungaji bora wa muda wote ndani ya ligi akiwa kafunga mabao zaidi ya 100 wakaibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Ipo wazi kuwa kwa msimu wa 2023/24 Simba ilipishana na mataji yote ambayo yapo mikononi mwa watani zao wa jadi Yanga ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Bara ambapo huko Yanga ilikusanya pointi 80 baada ya mechi 30 ikiwa nafasi ya kwanza na Simba iligotea nafasi ya tatu kwenye msimamo itatpeperusha bendera ya Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho.
Meneja Ally ameweka wazi kuwa bado mwendo ambao wanakwenda nao hawajafika hata robo ikiwa ni mwanzo tu wa msimu huku kila mchezaji akitimiza majukumu yake kwa umakini.