MCAMEROON KUCHUKUA MIKOBA YA LWANGA SIMBA
WAKATI wakijua kuwa wataachana na kiungo wao mkabaji, Taddeo Lwanga, uongozi wa Simba upo kwenye mawindo makali ya kumchukua kiungo Cedric Zemba Ekong raia wa Cameroon ili azibe pengo hilo. Simba wanataka kuliboresha eneo lao la ukabaji ambapo Ekong anayeitumikia Apejes FC ya kwao akifanywa kuwa chaguo namba moja. Kikosi hicho kwa msimu huu kimekuwa…