
AZAM FC WANAUTAKA UBINGWA WA KOMBE LA FA
KOCHA Mkuu wa Azam raia wa Marekani, Abdi Hamid Moallin ameweka wazi kuwa kipaumbele chake kikubwa mara baada ya kurasimishwa kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho, ni kuhakikisha wanashinda ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam (FA) linalotetewa na Simba. Moallin alitangazwa rasmi kuchukua majukumu ya ukocha mkuu ndani ya kikosi chaAzam Januari 25, mwaka huu mara baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa mafanikio kama kaimu kocha mkuu tangu…