
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumanne
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumanne
AHMED Ally, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa kwa sasa mpango mkubwa ni kuelekea kwenye mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Orlando Pirates unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo VAR itatumika kwenye mchezo huo na namna ambavyo itafungwa kwa kuwa tayari vikao vimeanza kufanyika.
UONGOZI wa Yanga umetumia mitetemo ya Fiston Mayele kuwatisha wapinzani wao wajao kwenye ligi ambao watakuwa ni Simba. Yanga inaongoza ligi ina pointi 51 baada ya kucheza mechi 19 bila kupoteza huku Simba ambao ni mabingwa watetezi wakiwa na pointi 41 baada ya kucheza mechi 19. Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa uwepo…
UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kwa sasa akili zao ni kuelekea mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Orlando Pirates. Aprili 17,2022 Simba itakuwa na mchezo wa kusaka ushindi dhidi ya Orlando Pirates Uwanja wa Mkapa unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari,Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema…
BADO Manchester City ni vinara wa Ligi Kuu England wakiwa wametofautiana pointi moja na wapinzani wao Liverpool. Zote zimecheza jumla ya mechi 31 ndani ya Ligi Kuu England msimu wa 2021/22 ambao ushindani wake ni mkubwa. Ni pointi 74 zipo kibindoni huku Liverpool wakiwa na pointi 73 kibindoni na ni mechi 22 wameshinda Liverpool huku…
KIUNGO mshambuliaji wa Klabu ya Simba raia wa Ghana, Bernard Morrison sasa ni rasmi kuwa hawezi kwenda nchini Afrika Kusini kutokana na kufungiwa kuingia ndani ya nchi hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo Barbara Gonzalez amethibitisha hilo rasmi kuwa jitihada zilizofanyika za kumuombea kibali cha kuingia nchini Afrka Kusini zimegonga mwamba. Barbara amesema:“Tuliwasiliana na watu…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumatatu
YANGA inatinga hatua ya nusu fainali baada ya ushindi wa penalti 7-6 mbele ya Geita Gold. Dakika 90 zilikamilika kwa timu zote kufungana bao 1-1 katika mchezo wa robo fainali Kombe la Shirikisho. Katika mchezo wa leo,Kocha Mkuu Nasreddine Nabi ameonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi wa kati baada ya kupuliza kipyenga cha mwisho. Sasa Yanga…
DAKIKA 45 za burudani safi kabisa kutoka kwa timu zilizofanya maandalizi mazuri kutimiza kile ambacho wamepewa na benchi la ufundi. Ubao wa Uwanja wa Mkapa unasoma Yanga 0-0 Geita Gold ikiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali. Timu zote zinapambana kusaka ushindi huku umakini ukiwa ni tatizo kwenye kumalizia nafasi. Zawadi…
UWANJA wa Ushirika Moshi,milango kwa timu zote mbili ilikuwa migumu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo na kufanya timu zote zigawane pointi mojamoja. Ubao umesoma Polisi Tanzania 0-0 Simba ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa 19 msimu wa 2021/22. Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara sasa wanafikisha pointi 41 wakiwa wameachwa kwa jumla ya pointi…
Simba sc na Cape Town City, zimefikia Makubaliano ya kuuziana Beki wa Kati raia wa DRC Congo Nathan Idumba Fasika, Uhamisho wa Nyota huyo unakadiliwa kukamilika mwishoni mwa msimu ili kumpa nafasi Idumba amalize kuitumikia Cape Town City kwa Msimu huu. kinachoendelea sasa ni Makubaliano binafsi na Beki huyo juu ya Mshahara wake na Simba…
NDANI ya Ligi Kuu England Manchester City ni baba lao kwa kukusanya pointi nyingi tangu msimu wa 2018/19 mpaka msimu huu wa 2021/22. Ni pointi 338 wamekusanya huku wanaowafuata wakiwa ni Liverpool ambao wana jumla ya pointi 337 na Chelsea ni namba tatu wakiwa na pointi 264 Manchester United ni namba nne wana pointi 257….
MENEJA wa Simba Queens inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite (SWPL), Selemani Makanya, amesema wachezaji wamejiandaa vema kuikabili Ruvuma Queens katika mchezo wa ligi hiyo utakaochezwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea. Akizungumza na Spoti Xtra, Makanya alisema: “Tunamshukuru Mungu tumefika salama, tumejiandaa vya kutosha kwa ajili ya mchezo huu, hakuna…
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ ameishukuru Benki ya NBC kwa kutoa motisha kwa wachezaji, huku akiamini hiyo inasaidia kujituma zaidi uwanjani. Saido aliyasema hayo baada ya hivi karibuni kupokea tuzo yake ya Mchezaji Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu Bara msimu huu sambamba na shilingi milioni moja kutoka kwa wadhamini wa…
MABAO kutoka kwa Leandro Trossard dk 28 na Enock Mwepu dk 66 yaliweza kutosha kuipa pointi tatu Brighton mbele ya Arsenal. Ni bao la Martin Odegaard dk 89 Uwanja wa Emirates lilitosha kuwafuta machozi washika bunduki hao wanaonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta. Arteta amesema kuwa walikuwa wana kila kitu cha kuweza kushinda lakini haikuwa…
UONGOZI wa Yanga SC, umefunguka kuwa, unayahitaji makombe yote wanayoshiriki msimu huu ambayo ni Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikiso la Azam Sports (ASFC). Leo Jumapili, Yanga wanatarajiwa kukipiga dhidi ya Geita katika mchezo wa robo fainali ya ASFC, unaotarajiwa kufanyika Uwanja wa Mkapa, Dar. Akizugumza na Spoti Xtra, Mjumbe wa Kamati ya…