
YANGA HAISHIKIKI, MAYELE AWEKA REKODI CAF,PHIRI HAPOI
YANGA haishikiki, Mayele aweka rekodi CAF, Zalan wapigwa kama ngoma, Simba v Big Bullets, njooni muone shoo, huyo Phiri hapoi ndani ya Spoti Xtra, Jumapili.
YANGA haishikiki, Mayele aweka rekodi CAF, Zalan wapigwa kama ngoma, Simba v Big Bullets, njooni muone shoo, huyo Phiri hapoi ndani ya Spoti Xtra, Jumapili.
Turejee kutoka kwa mbobevu wa simulizi za Eskimo bwana Knud mpaka kwenye uhalisia wa ushindi wa kasino ya Mtandaoni kwenye Book of Eskimo, kutoka Expanse Studio, pale Meridianbet. Bila shaka kila mmoja anapenda kusikia watu wakismuliana stori kuhusu uthubutu wake na ushujaa alionao – ila hii haitokei pale usipokuwa mshindi! Kasino ya Meridianbet inakusogeza…
NAMUNGO FC imesepa mazima na pointi tatu mbele ya Coastal Union kwa ushindi wa bao 1-0. Kwenye mchezo huo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Majaliwa ni bao la Relliats Lusajo dakika ya 38 limetosha kuipa ushindi. Ni kwa mkwaju wa penalti Lusajo amefunga ikiwa ni bao lake la kwanza kufunga kwa penalti baada ya yale…
MWENDO wa Geita Gold kimataifa umegota mwisho leo Septemba 17,2022 baada ya kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Hilal Al Sahil SC. NI faida ya bao la ugenini wanapata wapinzani wa Geita Gold ambao mchezo wa kwanza uliochezwa ugenini walishinda kwa bao 1-0. Juma ni mabao 2-2 wanakuwa wamefungana na kuifanya Geita Gold kufungashiwa virago…
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga ambao wanaiwakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wameibuka na ushindi mkubwa wa mabao 5-0 dhidi ya Zalan FC. Ni kwenye mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwafanya washinde kwa jumla ya mabao 9-0 dhidi ya Zalan FC ukiwa ni ushindi mkubwa kutokea kwa hivi…
RELLIATS Lusajo kasi yake ya kucheka na nyavu imezidi kushika kasi baada ya leo kupachika bao lake la tano ndani ya Ligi Kuu Bara. Ni mbele ya Coastal Union dakika ya 38 kwa mkwaju wa penalti kwenye mchezo unaochezwa Uwanja wa Majaliwa,Ruangwa, Lindi. Mzawa huyo kwa sasa ni namba moja kwa kucheka na nyavu akiwa…
UWANJA wa Mkapa, mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya awali ubao unasoma Yanga 0-0 Zalan, FC. Hakuna mbabe kwa timu zote mbili kwa sasa ndani ya dakika 45 huku Yanga ikionekana kuanza kwa kasi kuliandama lango la Zalan FC. Mashuti 8 Yanga wamepiga hajalenga lango huku Zalan FC wao wakipiga shuti moja ambalo…
KIKOSI cha Yanga kitakachoanza dhidi ya Zalan FC, Uwanja wa Mkapa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali, Septemba 17,2022:- Diarra Kibwana Lomalisa Bangala Job Feisal Sure Boy Moloko Mayele KI Aziz Farid Mussa Akiba Mshery Bacca Mwamnyeto Bryson Mauya Gael Nkane Yusuph Makambo
NYOTA wa Yanga Tuisila Kisinda ameanza mazoezi ndani ya kikosi cha Yanga akiwa na mchezaji Yacouba Songne tayari kwa msimu wa 2022/23
KOCHA Msaidizi wa Geita Gold, Mathias Wandiba ameweka wazi kuwa makosa ambayo waliyafanya kwenye mchezo wa kwanza wameyafanyia kazi leo watayarekebisha. Jana Septemba 16, 2022 Geita Gold ilifanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Azam Complex kujiweka sawa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Hilal Al Sahil. Kwenye mchezo wa kwanza wakiwa…
NAHODHA Msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Nyassa Big Bullets unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda itaingia uwanjani ikiwa na faida ya mabao 2-0 ambayo waliyapata ugenini na ina rekodi ya kutolewa na Jwaneng Galaxy Uwanja wa Mkapa…
VITA ya ufungaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara yakolezwa kati ya Moses Phiri na Mayele Fiston
NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa mastaa wake wanne wanatarajia kukosekana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Zalan FC ya Sudan Kusini. Djuma Shaban, Khalid Aucho, Bernard Morrison na Joyce Lomalisa hawa wanatarajia kuwakosa Wasudan hao. Leo Jumamosi, Uwanja wa Mkapa Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa…
STAA wa Manchester City Erling Haaland ametajwa kuwa Mchezaji Bora Premier katika mwezi Agosti, (mwezi uliopita). Mshambuliaji huyo Mnorway ametwaa tuzo hiyo baada ya kuanza vyema maisha yake kwenye Premier, akitimiza majukumu yake kwa kuifanya City kutokufungwa hadi sasa katika ligi hiyo. Wampeta ushindi dhidi ya West Ham United, AFC Bournemouth, Crystal Palace, Nottingham Forest…
UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa umempa mkataba wa muda kocha Juma Mgunda na hatma yakeipo kwa kocha mpya ambaye atakuja kukinoa kikosi hicho hivi karibuni. Mgunda amekabidhiwa timu na mabosi wa Simba baada ya kutangaza kuachana na Mserbia, Zoran Maki ambaye alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi za Ligi Kuu Bara na alishinda zote. Maki ametangazwa…
MWAMBA huyu hapa, Nabi achekelea Kisinda kuruhusiwa, amuingiza kikosi cha kwanza, Simba:Tunawashushia Wamalawi full mziki, Inonga ashusha presha
Meridianbet wameunga mkono jitihada za kampeni ya Buku ya Hedhi salama inayoratibiwa na Shufaa Hemed Nasoro. Kampeni hii ilikuwa imelenga kuchangisha michango ya kiwango cha angalau shilingi elfu moja kuwasaidia mabinti ambao wanapata changamoto za kumudu gharama za taulo za kike. Meridianbet, ambao ni wadau wakubwa wa shughuli za kijamii, wanaona umuhimu wa hedhi salama…