Home Sports NAMUNGO YASEPA NA POINTI ZA COASTAL UNION

NAMUNGO YASEPA NA POINTI ZA COASTAL UNION

NAMUNGO FC imesepa mazima na pointi tatu mbele ya Coastal Union kwa ushindi wa bao 1-0.

Kwenye mchezo huo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Majaliwa ni bao la Relliats Lusajo dakika ya 38 limetosha kuipa ushindi.

Ni kwa mkwaju wa penalti Lusajo amefunga ikiwa ni bao lake la kwanza kufunga kwa penalti baada ya yale manne kufunga kwenye mwendo wa kawaida.

Jumla Lusajo anafikisha mabao matano ambayo timu hiyo imefunga kwenye mechi nne na imefikisha pointi 10.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu huku nafasi ya kwanza ikiwa kwa Yanga na ile ya pili mikononi mwa Simba zote zina pointi 10 tofauti ya mabao ya kufunga na kufungana.

Previous articleGEITA GOLD WAMEUMALIZA MWENDO KIMATAIFA
Next articleKUTOKA KWENYE SIMULIZI ZA KNUD, MPAKA KWENYE USHINDI MKUBWA MERIDIANBET!