UONGOZI wa Simba SC umeweka wazi kuwa haujui wapinzani wao Pamba Jiji FC wamepata wapi nauli ya kupanda ndege kutokana na uwezo walionao jambo ambalo limeongeza ushindani mkubwa.
Juni 14,2026 ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Simba SC 2-1 Pamba Jiji FC, Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema alipoona wapinzani wao wamepanda ndege wakajua kazi wanayo.
Magoli ya Simba SC kwenye mchezo huo yalifungwa na Ellie Mpanzu na Libase Gueye huku lile la Pamba Jiji FC likifungwa na Mathew.
Ahmed amesema: “Nilipoona wapinzani wetu wamepanda ndege nikajua kazi tunayo kwa kuwa tunajua uwezo wao labda wameuza sato wamepata pesa lakini wanapaswa kumshukuru aliyewapa nauli.
“Kupanda kwao ndege kumepunguza umbali na badala ya kutumia saa zaidi ya 3 barabarani wametumia saa 1 wakiwa angani na kufika Dar, hakika wameonyesha kazi kubwa na ushindani mkubwa.
“Ila kupanda ndege halafu ukaacha pointi 3 kuna maumivu ambayo yapo hivyo wanapaswa kumshukuru yule aliyewapa nauli, tunawajua uwezo wao,” aliongea Ahmed muda mfupi baada ya mchezo kukamilika.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.