
LAKINI SIMBA MNA UHAKIKA TATIZO NI ROBERTINHO?
MWANAMUZIKI mkazi wa mkoani Morogoro, Selemani Msindi ‘Afande Sele’ aliwahi kuimba ‘kama hip-hop itakufa ni nani anapaswa kuchunwa ngozi? Je, ni Producer, mapromota au wasanii?’ Tungo hii ilikuwa na ujumbe kuwa ni lazima atafutwe wa kuwajibika kutokana na kudorora na ikitokea mziki huo wa ‘kufokafoka’ ukafa, hasa baada ya mziki wa aina ya Bongo Fleva…