MKANDAJI KAKANDWA KARIAKOO DABI NYUMBANI

    ASIYEKUBALI kushindwa si mshindani wanasema hivyo. Ilikuwa ni jasho la kazi kwa wanaume 22 kusaka ushindi Uwanja wa Mkapa na mwisho ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga.

    Wakandaji Simba wakiwa nyumbani walikandwa na wapinzani wao Yanga kwenye msako wa pointi tatu muhimu.Hapa  tunakuletea namna kazi ilivyokuwa namna hii:-

    Aishi Manula

    Mchezo wake wa kwanza ndani ya Simba msimu wa 2023/24 baada ya kuwa kwenye maumivu kwa muda mrefu. Aliokoa hatari dakika ya 27, 40, 41, 42, 70 alitunguliwa mabao matano.

    Dakika ya tatu, 64, 73, 77 na 87. Alikomba dakika 90 akishuhudia wakiyeyusha pointi tatu mazima. Alipiga pasi ndefu dakika ya 27, 32.

    Inonga

    Henock Inonga aliokoa hatari dakika ya 11, 28, 51, 62 alipiga pasi ndefu dakika ya 14, 15, 16, 59 alichezewa faulo dakika 22.

    Kapombe

    Shomari Kapombe beki wa Simba alipewa majukumu ya kurusha dakika ya 12, 13, 14, 22 aliokoa hatari dakika ya 40. Alipiga krosi dakika ya 4, 43, 45.

    Ntibanzokiza

    Saido Ntibanzokiza alipiga faulo dakika ya 49, alipiga pasi fupi dakika ya 4, alichezewa faulo dakika ya 6, 14, alipiga kona dakika ya 8.

    Che Malone

    Beki wa kazi aliokoa hatari dakika ya 17, 20, 25, 45 alicheza faulo dakika ya 85 akaonyeshwa kadi ya njano.

    Ngoma

    Fabrince Ngoma aliokoa hatari dakika ya 13, 16, 60, 68 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 22 baada ya kucheza faulo.

    Kibu

    Kibu Dennis alifunga bao moja dakika ya 8, alichezewa faulo dakika ya 38, alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango dakika ya 19, 32 aliokoa hatari dakika ya 24.

    Alikomba dakika 59 baada ya kupata maumivu nafasi yake ikachukuliwa na Luis Miquissone.

    Chama

    Clatous Chama alipiga faulo dakika ya 7, 39, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 7 alicheza faulo dakika ya 56 alipoonyeshwa kadi ya njano.

    Mohamed Hussein Zimbwe Jr

    Aliokoa hatari dakika ya 28, 44 alirusha dakika ya 15

    Hawa hapa wachezaji wa Yanga:-

    Djigui Diarra aliokoa hatari dakika ya 6, 7, 16 alipiga pasi ndefu dakika 16. Alifungwa bao moja dakika ya 8.

    Pacome Zouzoah aliokoa hatari dakika ya 21, alipiga pasi fupi dakika ya tatu, pasi ndefu ilikuwa dakika ya 19, 26 alifunga bao moja kwa pigo la penalti dakika ya 87.

    Kennedy Musonda alipachika bao la kwanza dakika ya tatu kwa pigo la kichwa akiwa ndani ya 18 alikomba dakika 71 aliingia Clement Mzize alitoa pasi ya bao dakika ya 73 na 77.

    Yao

    Yao Attohoula alipiga pasi ya bao dakika ya tatu akiwa nje ya 18, alicheza faulo dakika ya 16.

    Aucho

    Khalid Aucho aliokoa hatari dakika ya 4, 13, 14, 35 alipiga pasi mdefu dakika ya 15 aliokoa hatari dakika ya 17.

    Job

    Dickson Job aliokoa hatari dakika ya 20, 58, 60 alicheza faulo dakika ya 44, alichezewa faulo dakika ya 56 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 6.

    Maxi Nzengeli alipiga pasi fupi dakika ya 13, alicheza faulo dakika ya 16, alifunga mabao mawili dakika ya 64, 77.

    Mudhathir Yahya alipiga pasi ndefu dakika ya 14 alichezewa faulo dakika ya 43.

    Aziz KI alipiga pasi fupi dakika ya 18, 34 alipiga pasi ndefu dakika ya 26, 27 alifunga bao dakika ya 73.

    Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, (Dizo Click) na kutoka gazeti la Spoti Xtra Jumanne.

    Previous articleOGOPA MAPAPELI SALAH HAUZWI
    Next articlePESA ZINAMIMINIKA LEOUSIKU MECHI ZA UEFA, PIGA MKWANJA