Home Sports GAMONDI MASTA KUWABADILISHIA MBINU WAPINZANI

GAMONDI MASTA KUWABADILISHIA MBINU WAPINZANI

MIGUEL Gamondi Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa anaingia uwanjani kulingana na aina ya wapinzani ambao atakutana nao ndani ya dakika 90.

Novemba 5 Yanga ilikomba pointi tatu mazima dhidi ya watani zao wa jadi Simba kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga. Pointi tatu kibindoni na kutibua rekodi ya Simba kucheza mechi saba za msimu wa 2023/24 bila kufungwa kuendelea.

Kituo kinachofuata kwa Yanga ni Tanga, Novemba 8 Uwanja wa Mkwakwani kusaka pointi tatu dhidi ya Coastal Union ikiwa ni mchezo wa ligi.

 Gamondi amesema kuwa wanatambua kwamba kazi kubwa kwenye mechi zao zote ni kusaka ushindi wakibadili mbinu kulingana na mchezo husika.

“Kila mchezo unakuja kulingana na aina ya wapinzani ambao tunakutana nao. Tunatambua namna ushindani ulivyo hilo lipo wazi hivyo tunaingia uwanjani tukiwa na mpango kazi wa kusaka ushindi.

“Kikubwa ni kuona kwamba tunacheza vizuri na kuwapa burudani mashabiki wetu ambao wanajitokeza uwanjani. Wazidi kuwa pamoja nasi kazi bado ipo na tunaamini tutafanya vizuri,” amesema Gamondi.

Previous articlePESA ZINAMIMINIKA LEOUSIKU MECHI ZA UEFA, PIGA MKWANJA
Next articleMABORESHO YA VIWANJA MUHIMU KWA MWENDELEZO WA BURUDANI