
SIKU 10 ZIMETIMIA, MBALI NA MABANGO, MAPUMZIKO YANATUMIKAJE?
LEO Jumatano zimetimia siku 10 tangu wadau wa soka Tanzania na wapenzi wa timu za Simba na Yanga kupata mshtuko, kufuatia mashindano ya kushangaza ya dabi ya Kariakoo ambapo mchezo huo ulishuhudiwa ukimalizika kwa Simba kupokea kipigo cha mabao 5-1. Nimesema yalikuwa matokeo ya kushtusha hasa kwa kuwa mchezo huu kwa kawaida unakuwa na upinzani…