Home International HAWA HAPA MABINGWA WA AFL

HAWA HAPA MABINGWA WA AFL

Mabingwa wa African Football League ñi Mamelod Sundown ya Afrika Kusini mbele ya Wydad Casablanca.

Katika fainali ya leo ubao umesoma Mamelod 2-0 Wydad na kuwafanya watwae ubingwa kwa jumla ya mabao 3-1.

Bao la Peter Shalulile dakika ya 45 liliwaongezea nguvu vijana hao ambao walipachika bao ka pili dakika ya 53 kupitia kwa Modiba.

Haya ni mashindano mapya ambayo yameanza kwenye bara la Afrika kwa kujumuisha timu 8 ambazo zilianzia hatua ya robo fainali.

Kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na kati Simba ilipata nafasi ya kushiriki na iligotea hatua ya robo fainali kwa kufungashiwa virago na Al Ahly ya Misri.

Previous articleYANGA YARIPOTIWA KUMSAJILI KIUNGO MKATA UMEME WA IVORY COAST
Next articleSIMBA WAIREJESHA TUZO KWA MASHABIKI