
YANGA WAPANIA KUVUNJA REKODI KWA SIMBA
KOCHA Mkuu wa Yanga Princess, Edna Lema ‘Morinyo’ ameweka wazi kuwa anataka kufuta uteja mbele ya Simba Queens kwa kushinda kwenye mechi yao ya dabi itakayopigwa leo Jumamosi Januari 8 2022 katika Uwanja wa Mkapa, Dar. Kocha huyo alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano kati ya timu hizo na Waandishi wa Habari uliofanyika jana Ijumaa katika Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Edna amesema: “Sina matokeo mazuri au Yanga Princess haina matokeo mazuri mbele ya Simba, ila huu ni mchezo na matokeo ni baada ya…