
NYOTA MAN UNITED AWA MUUZA SAA
MANCHESTER, England NYOTA wa zamani wa Manchester United, Ramon Calliste ambaye alitamba utotoni na akina Cristiano Ronaldo na Wayne Rooney, ameliacha soka na kuwa muuza saa za kisasa. Calliste alikuwa akitajwa kama Ryan Giggs ajaye, alitamba katika timu ya vijana ya United. Hata hivyo, jeraha baya la enka alilopata mwaka 2006, lilimlazimisha astaafu soka mapema….