Home Sports AZIZ KI ATAJWA KUINGIA RADA ZA YANGA

AZIZ KI ATAJWA KUINGIA RADA ZA YANGA

 IMEELEZWA kuwa Yanga ipo kwenye mpango wa kuinsa saini ya kiungo mshambuliaji wa ASEC Mimosas Aziz Ki ili aweze kuongeza nguvu kwa msimu ujao wa 2022/23.

Nyota huyo alikuwa anapigiwa hesabu pia na Simba ambayo kwa sasa ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola baada ya Pablo Franco kuchimbishwa ndani ya kikosi hicho.

Ni Yacouba Songne huyu raia wa Burkina Faso, anatajwa kuweza kuwa sababu ya kiungo huyo kuweza kutua ndani ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

“Yacouba ni sababu ya kiungo huyo kuweza kuja Yanga hivyo muda huu wapo kwenye mazungumzo na Aziz ili aweze kuja kucheza ndani ya timu hiyo,” ilieleza taarifa hiyo.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga hivi karibuni alisema kuwa watafanya usajili makini kwa ajili ya msimu ujao.

Previous articleMORRISON AGOMEA KURUDI SIMBA,YANGA YATAJWA
Next articleKUMBE!CHAMA HAKUTAKIWA KUSAJILIWA SIMBA