Home Sports MASAU BWIRE:TUPO KWENYE NAFASI MBAYA

MASAU BWIRE:TUPO KWENYE NAFASI MBAYA

OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameweka wazi kwamba wapo kwenye nafasi mbaya katika ligi jambo ambalo haliwaridhishi kuwa hapo walipo kwa sasa.

Kwenye msimamo Ruvu Shooting ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 28 baada ya kucheza mechi 26 msimu huu huku safu yake ya ushambuliaji ikiwa imefunga mabao 24.

 Bwire amesema kuwa ugumu wa ligi unawafanya wazidi kupambana na wana amini kwamba watarejea kwenye ubora wao.

“Tuko kwenye nafasi mbaya na hatujaridhishwa kuwa katika nafasi huyo kwa sababu sio nzuri kabisa na kamwe hakuna mtu anayeridhishwa na kitu kisicho kizuri hivyo tutazidi kupambana.

“Kushindwa kupata matokeo mazuri haina maana ya kuwa timu haijitumi au shida ipo kwa walimu wao ila inatokea hivo kwa sababu ya ligi kuwa ngumu na kuwa ya ushindani wa hali ya huu hivyo kila timu inahitaji kupata ushindi ili iwe katika nafasi nzuri,” amesema Bwire.

Mchezo uliopita Ruvu Shooting iliweza kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mabatini.

Previous articleKUMBE!CHAMA HAKUTAKIWA KUSAJILIWA SIMBA
Next articleSINGIDA BIG STARS WAFUNGUKIA USAJILI WA BEKI SIMBA