Historia! Tanzania Yaweka Rekodi CAF – Timu Nne Zatinga Makundi
Kwa mara ya kwanza katika historia, Tanzania imefanikiwa kupeleka timu nne kwenye hatua ya makundi ya michuano inayoendeshwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Baada ya Simba SC kupata ushindi wa jumla wa 3-0 dhidi ya Nsingizini Hotspurs FC ya Eswatini, Wekundu wa Msimbazi wamejiunga rasmi na Yanga SC katika hatua ya makundi ya Ligi…