MWAMBA HUYU HAPA KUTUA YANGA,YEYE NI BEKI
IMEELEZWA kuwa Yanga ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya nyota Joyce Lomalisa ambaye anakipiga Klabu ya Sagrada Esperanca ya Angola. Nyota huyo ni beki ambaye anakuja kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi. Hivyo kutua kwake ndani ya Yanga kutafanya aweze kuungana na beki mwingine wa kazi, Yannick Bangala…