Home Sports CHEKI VIGONGO VYA KAZI ZA MATOLA SIMBA

CHEKI VIGONGO VYA KAZI ZA MATOLA SIMBA

SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba ana vigongo vitano ndani ya Juni kuweza kuiongoza timu hiyo kukamilisha mzunguko wa pili.

Mabingwa hao watetezi hawana uhakika wa kuweza kutetea taji hilo kutokana na kuachwa kwa pointi 13 na watani zao wa jadi Yanga walio nafasi ya kwanza na pointi 64.

Ni mechi za kazi ambazo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu hizo kuweza kuhitaji pointi tatu kama ambavyo Simba wanahitaji pia.

Itakuwa Juni 16,Simba v Mbeya City, Uwanja wa Mkapa,Juni 21, Simba v Mtibwa Sugar, Juni 26, Tanzania Prisons v Simba, Uwanja wa Sokoine na atafunga kigongo cha nne Juni 29 itakuwa Mbeya Kwanza v Simba, Uwanja wa Majimaji.

Ni mchezo dhidi ya KMC huu unatarajiwa kupingwa tarehe 19 Uwanja wa Mkapa hiki ni kiporo.

Jana kikosi cha Simba kiliweza kufanya mazoezi Uwanja wa Bunju ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa kesho dhidi ya Mbeya City.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza, Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Paul Nonga.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa maandalizi yapo sawa na kila mechi kwao ni muhimu kupata matokeo.

Previous articleMPANGO WA BIASHARA WAKWAMA KAITABA
Next articleENGLAND WANAAMINI KWAMBA WATASHINDA KOMBE LA DUNIA