Kipa wa Manchester City na nahodha wa timu ya taifa ya Italia, Gianluigi Donnarumma, amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Alessia Elefante katika sherehe kubwa iliyofanyika nchini Italia.
Donnarumma (27) alimuoa Alessia katika kanisa la Chiesa Madre di San Giorgio Martire, lililopo Locorotondo, Italia, huku hafla hiyo ikihudhuriwa na mastaa mbalimbali wa soka.
Miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria ni kocha wa Manchester City Pep Guardiola, mshambuliaji Erling Haaland, Sandro Tonali, Paolo Maldini pamoja na Nicolò Barella.
Donnarumma na Alessia walianza uhusiano wao mwaka 2016 katika mji wao wa asili wa Castellammare di Stabia, karibu na Naples. Wawili hao tayari wana mtoto wa kiume aitwaye Leo, aliyezaliwa mwaka 2024.

Wanandoa hao walitangaza uchumba wao mwezi Mei kupitia ujumbe kwenye Instagram wenye maneno “Long-term contract signed” wakimaanisha wameingia kwenye mkataba wa maisha.
Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland, alihudhuria sherehe hiyo akiwa pamoja na mwenza wake Isabel Haugseng Johansen. Haaland amekuwa akionekana mara kwa mara katika matukio mbalimbali tangu Kombe la Dunia, ambako umaarufu wake uliongezeka kwa kiasi kikubwa.
Donnarumma alijiunga na Manchester City msimu uliopita akitokea Paris Saint-Germain (PSG) kwa ada ya takribani pauni milioni 26, na katika msimu wake wa kwanza alifanikiwa kusaidia timu hiyo kutwaa mataji ya FA Cup na League Cup.
