Azam FC vs Simba SC huyu hapa mshindi

MLINDA mlango namba moja wa Azam FC, Aishi Manula amesema kuwa timu ambayo itacheza kwa umakini leo na kutumia nafasi uwanjani ina nafasi kubwa kupata ushindi.

Leo Septemba 16, 2026 Azam FC vs Simba SC watamenyana Uwanja wa Azam Complex kwenye msako wa pointi 3 muhimu saa 1:00 usiku.

Manula amesema: “Timu itakayocheza vizuri kwa kufuata maelekezo ya kocha wake ndio itakayoibuka na ushindi kwani haijawahi kuwa mchezo rahisi Azam FC tunapokutana na Simba SC,” amesema Manula.

Azam FC kwenye msimamo ipo nafasi ya 3 imekusanya jumla ya pointi 14 baada ya kucheza jumla ya mechi 6 inakutana na Simba SC iliyo nafasi ya pili ikiwa na pointi 15 baada ya mechi 5.

Timu hizi zote mbili hazijapoteza pointi 3 ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani msimu wa 2026/27.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Kuvipata mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.

Buy Ganzi ya Maumivu Book by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar