KOCHA SIMBA APISHANA NA TUZO

KOCHA Mkuu wa Simba Abdelhak Benchikha amepishana na tuzo ya kocha bora baada ya kuingia kwenye tatu bora ya wale wanaowania tuzo hiyo.

Mrithi huyo wa mikoba ya Roberto Oliveira alikuwa kwenye chungu kimoja na Walid Regragui wa Morocco pamoja na Aliou wa Senegal.

Mwisho kwenye usiku wa tuzo  kocha bora kwa timu za wanaume ni Walid Regragui wa Morocco akiwazidi Abdelhak Benchika wa (USM Alger/Simba SC) na Aliou Cisse wa Senegal.

Kwa upande wa Tuzo ya kocha bora timu za wanawake imekwenda kwa Desiree Elis wa Afrika Kusini akiwazidi Reynald Pedros wa Morocco na Jerry Tshabalala wa Afrika Kusini.