Azam FC yatambulisha nyota mpya

Azam FC imekamilisha usajili wa kiungo Donovan Makoma rai awa Ufaransa kuwa katika kikosi hicho kuelekea msimu mpya wa 2026/27.

Nyota huyu amesajiliwa akitokea Klabu ya Birkirkara ya Ligi Kuu Malta ikiwa ni mwendelezo wa kuongoeza nguvu kwenye kikosi hicho.

Wengine ambao wametambulishwa Azam FC ni John Mano raia wa Sudan alitambulishwa Julai 21,2026 akitokea Klabu ya Al Akhdar ya Libya.

 Hassan Mubiru raia wa Uganda alitambulishwa katika kikosi cha matajiri wa Dar ikiwa ni ingizo jipya Julai 20,2026.

Mchezaji wa kwanza kutambulishwa Azam FC ni Kipre Jr ambaye amenunuliwa kutoka MC Alger.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.