Sporting CP Kuikabili Strasbourg Inayobeba Alama za Chelsea

Mechi hii ya leo Julai 20 dhidi ya Strasbourg itakuwa fursa muhimu ya kuona jinsi Sporting CP wanavyojenga upya kikosi chao baada ya msimu wa uhamisho wenye mabadiliko makubwa.

Chini ya kocha Rui Borges, ambaye ameonyesha matokeo ya kuvutia akiwa na kiwango cha ushindi cha asilimia 72 katika mechi 53 alizosimamia, timu inaingia msimu mpya ikiwa na changamoto ya kuziba mapengo yaliyoachwa na wachezaji muhimu waliohama.

Miongoni mwa waliohama, ni pamoja na kiungo Morten Hjulmand aliyehamia Atletico Madrid, pamoja na kijana Geovany Quenda aliyehamia Chelsea. Nyota wao wa zamani wa mashambuliaji, Viktor Gyökeres, naye aliondoka kuelekea Arsenal msimu uliopita, hivyo mzigo wa kufunga mabao sasa unabebwa zaidi na Luis Suárez, mshambuliaji wa Kolombia aliyeletwa kuchukua nafasi hiyo. Mechi dhidi ya Strasbourg itatoa dalili za jinsi mashambulizi ya Sporting yatakavyofanya kazi bila nyota huyo wa zamani wa Uswisi.

Kwa upande wa nyongeza, Sporting wameleta wachezaji kadhaa wapya wanaotarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza mbele ya mashabiki msimu huu, akiwemo Rodrigo Zalazar kutoka Braga, Sergi Altimira kutoka Real Betis, Silas Andersen kutoka Häcken, na Issa Doumbia kutoka Venezia. Anayevutia zaidi ni Jesse Derry, kijana aliyeletwa kutoka Chelsea jambo linaloongeza mvuto wa ziada kwenye mechi hii, ikizingatiwa kuwa Strasbourg wenyewe ni klabu dada ya Chelsea chini ya umiliki wa BlueCo.

Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Mechi hii pia ni fursa kwa Borges kupima muundo mpya wa ulinzi na kati ya uwanja, hasa akizingatia idadi kubwa ya wachezaji waliojiunga msimu huu zaidi ya wachezaji kumi na tatu wameongezwa kwenye kikosi kikuu.

Kwa vile Sporting wanaendelea kucheza kwenye michuano ya UEFA Champions League msimu ujao, uwiano kati ya wachezaji wazoefu kama Gonçalo Inácio, Ousmane Diomande na Hidemasa Morita, na vipaji vipya, utakuwa muhimu sana kuelekea msimu mzito ujao.

Kwa jumla, mashabiki wanaofuatilia mechi hii wanapaswa kuangalia zaidi ya matokeo pekee ni fursa ya kuona ni wachezaji gani wapya watakaoanza kuonyesha uwezo wao, na jinsi Rui Borges anavyopanga kuchanganya vipaji vipya na wachezaji wa zamani kabla ya msimu rasmi kuanza mwezi ujao.