Simba SC yatambulisha wapya wawili

KUELEKEA msimu wa 2026/27 Simba SC imetambulisha nyota wapya wawili ambao imekamilisha usajili ikiwa ni maandalizi kwa mechi zijazo za ushindani.

Simba SC itafungua mchezo wa kwanza wa NBC Premier League kwa kumenyana na Kagera Sugar , Agosti 16,2026 ikiwa ni mchezo wa kwanza kwenye msimu mpya.

Wachezaji wote wawili ambao wametambulishwa wametoka timu za ndani huku wengine wakitarajiwa kutambulishwa hivi karibuni.

Nashon

Kelvin Nashon kiungo mkabaji alitambulishwa Simba SC rasmi Julai 19,2026 akitokea Pamba Jiji FC.

Chilambo

Nathaniel Chilambo beki wa kulia alitambulishwa rasmi Julai 20 2026 kikosi cha Simba SC akitokea Azam FC.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.