Breaking: Yanga SC yatambulisha mshambuliaji mpya

RASMI mabingwa watetezi wa NBC Premier League wametambulisha mshambuliaji mpya ikiwa ni maandalizi kuelekea msimu wa 2026/27 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali.

Nyota huyu anakuwa wa pili kutambulishwa kutoka kwa watoto wa Jangwani ambao wamebainisha kwamba wamekamilisha usajili wa nyota wapya zaidi ya wawili.

Huyu anaitwa Hussen Mihambo aliyekuwa anakipiga ndani ya kikosi cha Mashujaa FC inayotumia Uwanja wa Lake Tanganyika kwa mechi zanyumbani.

Mchezaji mwingine ambaye ametambulishwa ni Juma Issa Abushir huyu alitambulishwa Julai 18,2026 yeye ni beki kutoka Fountain Gate maarufu kwa jina la Chuga Boy.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.