Meneja Mkuu Dimitar Pantev na Simba SC kibarua kimeota nyasi

RASMI Simba SC imefikia makubaliano ya kuachana na Dimitar Pantev ambaye alikuwa ni Meneja Mkuu wa timu hiyo.

Desemba 2,2025 taarifa rasmi kutoka Simba SC imeeleza kuwa wamefikia makubaliano ya pande zote mbili kuvunja mkataba.

Pantev alisaini mkataba wa miaka miwili kwa mujibu wa uongozi wa Simba SC hivyo mkataba wake haujafika hata muda wa mwaka mmoja.

Mchezo wa mwisho kwa Pantev kukaa benchi ilikuwa dhidi ya Stade Mallien ugenini na alishuhudia ubao ukisoma Stade Mallien 2-1 Simba SC hatua ya makundi.

Kwa sasa timu itakuwa chini ya Seleman Matola ambaye atakiongoza kikosi hicho kwenye mechi zijazo.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.