Home International MALI YATINGA ROBO FAINALI MBELE YA BURKINA FASO

MALI YATINGA ROBO FAINALI MBELE YA BURKINA FASO

TIMU ya taifa ya Mali anayocheza kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra iliwafungashia virago wapinzani wao Burkina Faso anayocheza Aziz KI anayecheza Klabu ya Yanga.

Ndani ya dakika 90 kwenye hatua ya 16 bora mshindi aliyetinga robo fainali ya Kombe la mataifa ya Afrika (Afcon) ni Mali baada ya kutinga Burkina Faso mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly Ivory Coast.

Mabao ya mchezo huo kwa upande wa Mali yamefungwa na Edmond Tapsoba aliyejifunga dakika ya tatu na Lassine Sinayoko dakika ya 47’ huku la Burkina Faso likifungwa na Betrand Traore 57 kwa mkwaju wa penalti akimpoteza mlinda mlango Diarra.

Kwa ushindi huo Mali itakutana na Ivory Coast Februari 3 katika robo fainali inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90.

Previous articleMITAMBO YA KAZI AZAM FC INAPIKWA UPYA
Next articleMOROCCO WAKUTANA NA MAAJABU YA AFRIKA KUSINI