Home Sports MOROCCO WAKUTANA NA MAAJABU YA AFRIKA KUSINI

MOROCCO WAKUTANA NA MAAJABU YA AFRIKA KUSINI

WABABE wa kundi F, lililokuwa na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars iliyoishia hatua ya makundi, Morocco wamefungashiwa virago katika Kombe la Mataifa Afrika, (AFCON) mbele ya timu ya Afrika Kusini.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Morocco 0-2 Afrika Kusini kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.

Mabao yalifungwa na Evidence Makgopa dakika ya 57, Teboho Mokoena dakika 90+5.

Ngoma itakuwa ni dhidi ya Cape Verde katika hatua ya robo fainali, Ivory Coast.

Wababe hao wamekutana na maajabu ya Afrika Kusini kwa kufungashiwa virago mapema walipokuwa wakipewa nafasi ya kufanya vizuri kwenye AFCON 2023.

Previous articleMALI YATINGA ROBO FAINALI MBELE YA BURKINA FASO
Next articleANAUZWA ULAYA BEKI WA KAZI BACCA?