KIWANGO cha beki wa kazi ndani ya Yanga Ibrahim Bacca kimekuwa gumzo kila kona huku makocha wakibainisha kuwa uwezo wake unamtosha kucheza Ulaya na akafikiamafanikio yake. Mbali na Bacca nyota Aziz KI na Djigui Diarra wote wa Yanga wanatajwa kuwa kwenye hesabu za kuibukia kwenye changamoto mpya.