UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa baada ya kuwa chimbo kwa muda mrefu wanarejea ndani ya Februari kutoa burudani mwanzo mwisho kwenye mechi ambazo watacheza kitaifa na kimataifa.
Ikumbukwe kwamba Simba mara ya mwisho kushuka uwanjani kwenye mechi za ushindani ilikuwa ni Januari 13 Uwanja wa Amaan uliposoma Mlandege 1-0 Simba, Kombe la Mapinduzi 2024.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa walikuwa kimya kwa muda mrefu wakifanya maandalizi kwa mechi zao zote hivyo wanarejea kuendeleza burudani mwanzo mwisho.
βIle burudani ambayo ilikosekana kwa muda inarejea na tupo tayari kwa ajili ya kuendeleza ule ubora ambao ulikosekana kwa muda mrefu. Kasi kubwa na morali kwenye kusaka ushindi upo hivyo Wanasimba ni muda wa kuwa tayari kwa jambo hili.
βKikubwa ni ushirikiano kwenye kila mechi kwani ushindani ni mkubwa. Benchi la ufundi linafanya kazi kubwa kuwapa mbinu wachezaji tunaamini tutafaya vizuri kwenye mechi zetu,β alisema Ally.
Kikosi cha Simba leo kinatarajiwa kushuka Uwanja wa Azam Complex kusaka ushindi kwenye raundi ya pili ya Kombe la AzamSports Federation dhidi ya Tembo FC.