PUMZIKA KWA AMANI NISHER

MTAYARISHA wa video za muziki Bongo, Nic Davie maarufu kwa jina la Director Nisher amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, saa nane na dakika tisa.

Taarifa za kifo cha Nisher zimethibitishwa na familia yao, ambapo kupitia akaunti za mitandao ya kijamii, wameandika.

“Familia ya Nabii Mkuu, Dkt. Geordavie inasikitika kutangaza kifo cha kijana wao mpendwa, Nic Davie kilichotokea usiku wa kuamkia leo, saa nane na dakika tisa…” imesomeka taarifa hiyo.

Director Nisher alipata umaarufu mkubwa baada ya kutengeneza video kali nchini Tanzania kama Jikubali ya Ben Pol na G-Nako, Mama Yoyoo ya G-Nako, video nyingi za Kundi la Weusi, Young Killer na wengine wengi.

Pumzika kwa amani Nisher