Home International YANGA YAGAWANA POINTI KIMATAIFA

YANGA YAGAWANA POINTI KIMATAIFA

IKIWA Uwanja wa du 26 Mars nchini Mali imeshudia ubao ukisoma Real Bamako 1-1 Yanga.

Mchezo wa leo ambao ni wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Yanga ilianza kupata bao la kuongoza dakika ya 60 kupitia kwa nyota wao Fiston Mayele.

Mayele alipachika bao hilo akiwa nje kidogo ya 18 na kuwanyanyua mashabiki wa Yanga pamoja na benchi la ufundi.

Zikiwa zimesalia sekunde mpira kugota mwisho kona ya Real Bamako ilileta bao kupitia kwa nyota wao Emile Kane dakika ya 90.

Yanga inagawana pointi mojamoja ugenini na inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi D ambalo vinara ni Monastir wenye pointi 7.

Previous articleREAL BAMAKO 0-0 YANGA KIMATAIFA
Next articleMANCHESTER UNITED YATWAA CARABAO