Home Uncategorized SIMBA YASEPA NA POINTI TATU KIMATAIFA

SIMBA YASEPA NA POINTI TATU KIMATAIFA

HATIMAYE kikosi cha Simba kimeibuka na ushindi kwenye mchezo wake wa kwanza hatua ya makundi ikiwa ugenini.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa St Mary’s umesoma Vipers 0-1 Simba na kuwafanya wasepena pointi tatu mazima.

Mtupiaji wa bao la ushindi ni Henock Inonga ambaye aliwapa furaha wachezaji wenzaki ikiwa ni pamoja na Kibu Dennis, Moses Phiri,Shomari Kapombe ambao ni baadhi ya walioanza kikosi cha kwanza.

Ni dakika ya 19 mashabiki wa Simba walinyanyuka kushangilia bao hilo ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Kwenye mechi mbili mfululizo Simba ilikwama kushinda wala kufunga bao ilikuwa dhidi ya Horoya na Raja Casablanca ambapo kwenye mechi hizo ilitunguliwa.

Previous articleKMC YAPOTEZA KWA MARA NYINGINE TENA
Next articleNABI:REAL BAMAKO NAWATAMBUA, MCHEZO UTAKUWA MGUMU