Home International NABI:REAL BAMAKO NAWATAMBUA, MCHEZO UTAKUWA MGUMU

NABI:REAL BAMAKO NAWATAMBUA, MCHEZO UTAKUWA MGUMU

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa anawafahamu wapinzani wake Real Bamako hivyo ataingia kwa tahadhari.

Leo Februari 26 Yanga inatupa kete yake ya tatu kwenye hatua za kimataifa katika Kombe la Shirikisho hatua ya makundi.

Kete ya kwanza Yanga ilipoteza ugenini dhidi ya US Monastir kisha ikpata ushindi dhidi ya TP Mazembe Uwanja wa Mkapa.

Nabi amesema:“Naifahamu Bamako, ni timu nzuri yenye wachezaji wazoefu, sitegemei utakua mchezo rahisi kwao na kwetu pia, naamini wachezaji wetu wako tayari kupambana kwa dakika 90.

“Mchezo utakuwa mgumu na ninawaheshimu wapinzani wetu ambao tunakutana nao na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu muhimu.”

Previous articleSIMBA YASEPA NA POINTI TATU KIMATAIFA
Next articleCHAMA KWENYE MTEGO, NABI AITEKA SHOO